Muhtasari wa Kipindi cha 16

Katika Kipindi cha 16, umejifunza kwamba:

  1. Hali hatari za kawaida zinazongeza chanzo cha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto wakati wa utunzaji katika ujauzito ni: chochote kilicho haribu kizuizi cha kawaida kinachotenganisha damu ya mama na ya fetasi katika plasenta, kama vile maambukizi kwa plasenta au kutokwa na damu, jeraha, kusugua vibaya fumbatio, utapiamlo kwa mama, na uvutaji sigara; mtoto kupatana na mchozo kutoka ukeni ulioambukizwa au damu ya mama wakati wa leba na kuzaa; na kupatana kwa muda mrefu na VVU kutoka kwa maziwa ya mama.
  2. UMKMM inatolewa kama sehemu ya kawaida ya huduma ya afya ya mama na ya mtoto. Ndio hatua ya kwanza katika huduma ya uzuiaji, matibabu, utunzaji na usaidizi kwa kina mama wajawazito wanaoishi na VVU, watoto wao, na washirika.
  3. Uchunguzi wa VVU na ushauri ni moja ya hatua ya kimsingi ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto. Zingine ni: kutoa dawa za kupunguza makali ya VVU kwa kina mama wanaoishi na VVU na watoto wachanga, utoaji wa huduma salama ya kuzaa, na ulishaji wa mtoto.
  4. Mbinu ya kutoshirikisha ya kushauri wa kuchunguza VVU ni bora zaidi kuliko mbinu ya kushirikisha na inapendekezwa na miongozo ya nchi nyingi Afrika.
  5. Uchunguzi wa Haraka wa VVU ndio unaotumika kawaida katika uchunguzi wa antibodi za VVU nchini Afrika na inafaa kwa uchunguzi wa kupima damu nyumbani na katika kituo cha Afya.
  6. Kuwepo kwa VVU lazima uthibitishwe na uchunguzi wa pili kwa kutumia kifaa cha kampuni nyingine. Iwapo uchunguzi wa pili inatofautiana na matokeo ya uchunguzi wa kwanza, uchunguzi wa tatu unapaswa kutekelezwa kwa kutumia Mwongozo wa Uchunguzi wa Haraka wa VVU (Kielelezo 16.2).
  7. Kina mama walio na VVU lazima wahimizwe sana kuzaa katika kituo cha afya cha ngazi ya juu ambapo mbinu za juu zaidi za Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto na dawa za kuzuia maambukizi za kiwango cha juu zaidi kuliko zile zinazopatikana kwa kawaida, zinanaweza kutolewa.
  8. Ushauri baada ya kuchunguza kwa kina mama wanaoishi na VVU na wale ambao hawana unapaswa kuwa ni pamoja na ushauri wa mazoea ya kufanya ngono salama, kuhimiza mume au mwenzi wa mama kuchunguzwa VVU, na umuhimu wa kupanga uzazi.
  9. Kina mama wajawazito wanaoishi na VVU watahitaji utunzaji na usaidizi zaidi unaoendelea, na rufaa na ufuatiliaji wao, watoto wao walio hatarini ya maambukizi, wenzi wao, na wengine katika familia.

16.8 Huduma ya ziada kwa mama anayeishi na VVU wakati wa ujauzito

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 16