Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 16

Kwa kuwa umekamilisha kipindi hiki, unaweza kutathmini jinsi ulivyofanikisha Malengo ya Somo kwa kujibu maswali haya. Andika majibu yako katika shajara yako ya somo na uyajadili na Mkufunzi wako katika Mkutano ujao wa somo la usaidizi. Unaweza kulinganisha majibu yako na Maelezo juu ya Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.

Swali la Kujitathmini 16.1 (linatathmini Malengo ya Somo 16.1)

Mama anafanya ngono na mtu aliye na VVU. Baada ya wiki mbili anafanyiwa uchunguzi wa maambukizi ya VVU. Matokeo yanaonyesha kutokuwepo VVU.

  • a.Je, utaamini matokeo haya? Toa sababu za jibu lako.
  • b.Unapaswa kufanya nini tena?

Answer

  • a.Hapana, hupaswi kuamini matokeo hayo. Huenda antibodi za mama hazijatokea tangu kuambukizwa, uchunguzi unaweza kutoa matokeo yasiyoonyesha kuwepo kwa VVU hata ikiwa ameambukizwa kufuatia ngono.
  • b.Mshauri mama aje kwa uchunguzi tena baada ya antibody kujitokeza, ambacho huchukua karibu wiki 12, na kutumia njia salama ya ngono ili kuhakikisha kwamba hapitishi VVU kwa mwingine ikiwa amepata maambukizi.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 16.2 (linatathmini Malengo ya Somo 16.2)

Hali nyingi huongeza hatari ya MKMM katika kipindi cha ujauzito. Nini hufanana kwa hali hizi mbili? Toa mifano miwili.

Answer

Hali mbili ni ufutaji wa sigara, na jeraha katika fumbatio, kwa mfano kutoka chombo kilichochongoka. (Kumbuka: Unaweza kuwa umechagua hali zingine kutoka zile zilizoorodheshwa katika Kisanduku 16.1.) Hali hizi hufanana kwa sababu zinaweza kuharibu kizuizi kati ya usambazaji wa damu kwa plasenta na fetasi na hivyo damu ya mama kuchanganyika na ya fetasi. Hii inaongeza hatari ya Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 16.3 (linatathmini Malengo ya Somo 16.3)

Mama mjamzito amekataa kuchunguzwa kwa VVU. Je, unaweza kufanya lolote?

Answer

Ikiwa mama mjamzito amekataa kuchunguzwa kwa VVU, unaweza:

  1. Kuchunguza ni kwa nini alikataa – anayo sababu maalum ya kukataa? Shughulikia maswala yoyote maalum na wasiwasi anayoweza kuwa nayo. Andika majadiliano hayo. Mshawishi ili akuamini na ushughulikie matatizo yake kwa makini, kwa mfano kuhusu athari kwa familia yake, uoga wa kuaibika na ubaguzi.
  2. Mhakikishie kwamba kukataa kwake kuchunguzwa haiathiri upatikanaji wa utunzaji katika ujauzito, utunzaji wa leba na kuzaa, utunzaji baada ya kuzaa, au huduma zinazohusiana.
  3. Kutoa ushauri kabla ya uchunguzi tena katika ziara ya ujauzito wa baadaye.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 16.4 (linatathmini Malengo ya Somo 16.4)

Je, ni manufaa gani kuu ya kutumia mbinu ya kutoshirikisha badala ya kushirikisha katika uchunguzi wa VVU?

Answer

Kwanza, kina mama wajawazito wengi wanaweza kukubali uchunguzi wa VVU ikiwa mbinu ya kutoshirikisha itatumika. Pili, kina mama wengi wakichunguzwa, uchunguzi wa VVU itaonekana kama jambo la kawaida na kukubali kama sehemu ya kawaida ya utunzaji katika ujauzito. Tatu, haichukui muda mwingi wa wahudumu wa afya, kwa sababu haihusishi muda mrefu wa ushauri kabla ya uchunguzi kwa kila mwanamke.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 16