16.2 Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto hutokea lini?

Ingawa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto inaweza kutokea wakati wa ujauzito, hatari kubwa ya maambukizi ni wakati wa leba na kuzaa. Hatari ya maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto (MKMM) wakati wa kunyonyesha, hutegemea namna na muda wa kunyonyesha.

Kabla ya kushughulikia, inakadiriwa kuwa kati ya watoto wachanga 40 kutoka 100 (40%) waliozaliwa na kina mama walio na VVU wataambukizwa. Jedwali 16.1 linaonyesha hatari ya maambukizi wakati wa ujauzito, leba na kuzaa, na wakati wa kunyonyesha. Asilimia sitini ya watoto wa kina mama walio na VVU hawatapata virusi hivi kamwe. Hata hivyo, sio rahisi kutabiri ni mama yupi atakayesambaza virusi kwa mtoto, hivyo ni lazima utoe huduma ya uzuiaji wa maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto kwa wajawazito wote walio na VVU

Jedwali 16.1 Asilimia iliyokadiriwa ya maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto (MKMM) wakati wa vipindi tofauti vya maambukizi.
Muda wa maambukiziHatari ya maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto (MKMM) bila suluhisho lolote
Wakati wa ujauzito (katika uterasi)5–10%
Wakati wa leba na kuzaa 10–15%
Wakati wa kunyonyesha baada ya kuzaa 5–10%
Hatari ya kijumla bila kunyonyesha15–25%
Hatari ya kijumla na kunyonyesha hadi miezi 620–35%
Hatari ya kijumla na kunyonyesha hadi miezi 18-2430–45%
Jumla ya hatari ya MKMM20–40%
Ilinukuliwa kutoka FMoH, 2007, Miongozo ya Uzuiaji wa Maambukizi kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto barani Afrika.
  • Kwa kuangalia data katika Jedwali 16.1, Kipindi cha unyonyeshaji huathiri vipi hatari ya MKMM?

  • Mtoto huwa katika hatari ya kuambukizwa VVU, akinyonyeshwa kwa muda mrefu. Ikiwa mtoto atanyonyeshwa hadi miezi 6 hatari ya kupata maambukizi ni 20-35%. Hatari huongezeka hadi 30-45% ikiwa mtoto atanyonyeshwa hadi umri wa miezi 18-24. Hii ni kupanda kwa 10% kwa hatari ya MKMM

    Mwisho wa jibu

Ikiwa maambukizi ya VVU inaweza kutambuliwa na kutibiwa kwa njia inayofaa katika kipindi cha utunzaji katika ujauzito, basi itapunguza uwezekano wa MKMM wakati wa leba na kuzaa au unyonyeshaji. Baada ya hapo, tutaangalia mambo ambayo huongeza hatari ya MKMM wakati wa ujauzito.

16.1 Uzuiaji wa Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto wakati wa Utunzaji katika Ujauzito

16.3 Vipengele vinavyongeza hatari ya maambukizi ya VVU wakati wa ujauzito