16.3 Vipengele vinavyongeza hatari ya maambukizi ya VVU wakati wa ujauzito

Virusi hupatikana kwa wingi katika njia ya uzazi (seviksi na ukeni) na kwa damu ya mama, kwa wajawazito walio na VVU. Kwa hivyo, ikiwa mtoto atakuwa wazi kwa viowevu vya ukeni au damu ya mama wakati wa leba na wa kuzaa, kuna chanzo kikubwa cha kutokea kwa MKMM.

Kawaida, hakuna mchanganyiko wa moja kwa moja kati ya damu ya mama na ya fetasi kwa uterasi, kulingana na Kipindi cha 5. Hata hivyo, chochote kitakachovunja kizuizi kati ya plasenta na ukuta wa uterasi kitazidisha hatari ya MKMM. Kisanduku 16.1 kinaorodhesha baadhi ya mambo ambayo wakati wa ujauzito yanaweza kudhuru kizuizi cha usambazaji wa damu kati ya mama na fetasi katika plasenta, na kuzidisha hatari ya MKMM. Utajifunza mengi kuhusu mambo ya hatari yanayoongeza chanzo cha Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto wakati wa leba na kuzaa, na wakati wa kunyonyesha, katika Moduli mbili zifuatazo za Utunzaji wa Leba na Kuzaa na Utunzaji baada ya kuzaa.

Kisanduku 16.1 Uharibifu wa kizuizi kati ya fetasi na mishipa ya damu yam am katika plasenta

Mambo ya kawaida ambayo huharibu kizuizi kati ya fetasi na mishipa ya mama katika plasenta na kuweka wazi fetasi kwa damu ya mama ni pamoja na:

  • Maambukizi ya plasenta kwa sababu ya malaria, na bakteria au virusi.
  • Plasenta kuvuja damu kabla ya leba (kuvuja damu kabla ya kuzaa). Hii hutokea kwa sababu ya kuachana kwa plasenta (plasenta kujiachilia kabla ya kutoka kwa uterasi) au plasenta privia (Plasenta inaofunika ufunguzi wa seviksi). Utajifunza mengi zaidi katika Kipindi cha 21.
  • Jeraha katika fumbatio kutokana na pigo, au vitu vilivyo na ncha ambavyo huingia kwa fumbatio.
  • Fumbatio kukandwa kwa nguvu na wauguzi wa kitamaduni baada ya miezi mitatu ya mimba. Katika baadhi ya maeneo ya Kusini mwa Jnagwa la Afrika, waganga wa kitamaduni hukanda fumbatio mara kwa mara, wakiamini itarahisisha uzalishaji.
  • Utapiamlo kwa wajawazito, hasa upungufu wa Vitamini C, A au madini ya zinc.
  • Uvutaji wa sigara, hudhoofisha membreni za fetasi na kuzunguka mtoto ambaye hajazaliwa na kuzidisha hatari ya kuachana kwa plasenta.

Swali unaloweza kuuliza ni je, mimba huathiri maendeleo ya ugonjwa wa VVU, au maendeleo ya ugonjwa wa VVU huathiri ujauzito. Hadi sasa, kuna ithibati kwamba mimba haizidishi VVU. Vile vile, hakuna ithibati kwamba maambukizi ya VVU husababisha matokeo mabaya ya mimba.

16.2 Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto hutokea lini?

16.4 UMKMM: maswala muhimu ya kuzingatia