16.4 UMKMM: maswala muhimu ya kuzingatia

Unapaswa kuwashawishi wajawazito wote wajitolee kuchunguzwa kwa VVU. Unaweza kutekeleza uchunguzi wewe mwenyewe (tazama Sehemu 16.5.1 hapa chini), lakini kama huwezi kutekeleza uchunguzi, uchunguzi huo hupatikana katika vituo vyote vya afya na hospitali. Mweleze mjamzito kwamba ikiwa atapatikana na VVU, anaweza kupata huduma bora ya kuzuia mtoto wake kutokana na VVU kabla au baada ya kuzaa. Pia mwambie kwamba kuna matibabu yake na mpenzi wake (ikiwa mpenzi wake atapatikana na VVU). Maswala muhimu ya UMKMM zilizozingatiwa zimetajwa katika Jedwali 16.2.

Profilaksisi (inatamkwa kama ‘proff-ill-aksisi’) inamaanisha ‘tiba linalolenga kuzuia’. Dawa za kupunguza makali ya VVU hutumiwa ili kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama aliye na VVU hadi kwa mtoto.

Kisanduku 16.2 Maswala muhimu ya kuzingatia katika UMKMM

  • Uchunguzi wa VVU na ushauri. Utajifunza mengi kuihusu katika kipindi hiki. (Ulijifunza kuhusu kanuni za kushauri za kijumla katika kipindi cha 15)
  • Kuwapatia wanawake wajawazito walio na VVU dawa za kupunguza makali. Dawa hizi hupigana na virusi kama vile VVU ambavyo ni ya 'familia' ya virusi iitwayo retroviruses. Hupewa kama sehemu ya tiba ya kupunguza makali kwa wanawake ambao wanastahili kuanza matibabu ya maambukizi ya VVU kwao, au tiba ya kupunguza makali ya virusi kwa wajawazito ambao hawastahili kuanza matibabu ya kurefusha maisha kwa wakati huu. Kuwapa wajawazito dawa za kupunguza makali ya VVU ama kabla au wakati wa ujauzito huwafaidi moja kwa moja, lakini pia husaidia kuzuia maambukizi ya VVU kwa mtoto. Kwa mujibu wa Miongozo ya VVU ya Uzuiaji wa Maambukizi kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto wa2007 ya Afrika, dawa za kuongeza maisha zinapaswa kuanzishwa katika wiki ya 28 ya ujauzito, lakini matibabu yake inaweza kuanza wakati wowote kama mwanamke anastahili. (Utajifunza kwa undani kuhusu vigezo vya ustahilivu tiba ya VVU katika Moduli ya Magonjwa Ambukizi).
  • Kutekeleza uzalishaji kwa njia salama. Hizi zimefunzwa katika Moduli ya Utunzaji wa Leba na Kuzaa.
  • Kutekeleza ulishaji wa mtoto kwa njia ya salama. Utajifunza kuhusu haya katika Moduli ya Udhibiti wa maradhi ya watoto wachanga na ya utotoni.

16.3 Vipengele vinavyongeza hatari ya maambukizi ya VVU wakati wa ujauzito

16.4.1 Dawa za kutibu na kupunguza makali ya VVU