16.4.1 Dawa za kutibu na kupunguza makali ya VVU

Dawa za kupunguza makali ya virusi ya kukinga maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto zinahusisha kumpatia mama dawa za kurefusha maisha kwanzia wiki 28 za ujauzito, pia kwa mama wakati wa leba na kuzaa, na kwa mtoto wake mara tu baada ya kuzaliwa. Dawa hizi hupunguza hatari ya maambukizi ya VVU kwa mtoto. Ni tofauti na tiba ya kupunguza makali ya virusi anayopewa mama ili kutibu maambukizi ya VVU, kulingana na uhakiki wa vigezo vyake.

Ikiwa mama aliye na VVU anapendelea na asisitize kuzaa nyumbani, dawa za kupunguza makali ya virusi za kisasa ambazo zinaweza kupatikana zinaitwa Nevirapine. Wakati utajua kwamba mama aliye na VVU yuko karibu kuzaa nyumbani, ikiwa umepewa mamlaka na umehitimu kufanya hivyo, unapaswa kumpa dozi moja ya Nevirapine (miligramu 200) ameze leba inapoanza. Ni bora ikiwa utatekeleza utambuzi wa leba na umpatie dawa wewe mwenyewe. Pia, mtoto anapaswa kupokea dozi moja ya Nevirapine baada ya siku 3 za kuzaliwa. Unapaswa kuwapa dawa hii moja kwa moja kulingana na uzito wa mtoto. Utajifunza kufanya hivi katika Moduli ya Magonjwa Ambukizi katika mtaala huu.

Kwa wale wanaozaa katika kituo cha afya au hospitalini, aina tatu ya dawa za kurefusha maisha zinapaswa kumezwa na kina mama walio katika leba kama profilaksisi (AZT + Neverapine + Lamuvudine). Mke na mumeo wanapaswa kujua kwamba aina hizo tatu za dawa zimezwapo wakati wa leba humkinga mtoto.

Aidha, mtoto atapewa dawa mbili (AZT + Lamuvudine) kwa wiki 1-4. Hivyo basi, unapaswa kuwashawishi kina mama walio na VVU kuzalisha katika vituo vya afya au hospitalini.

Dawa hizi za kupunguza makali ya virusi hupunguza hatari ya Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto, lakini hazitibu maambukizi ya VVU kwa mama wala haziboreshi afya yake. Wakati mwingine, mjamzito anaweza kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU ili kutibu VVU kabla ya kuzaa (iwapo anastahiki). Kwa hivyo, unapaswa kuwahimiza wajawazito wote walioambukizwa VVU kwenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu kuangalia kama wanaweza kuanza kunywa dawa za kupunguza makali ya VVU ambazo zitalinda watoto wao.

16.4 UMKMM: maswala muhimu ya kuzingatia

16.5 Utaratibu wa kuchunguza VVU wakati wa ujauzito