16.5.1 Kutambua maambukizi ya VVU kwa kutumia uchunguzi wa damu

Maambukizi ya VVU yanaweza kutambuliwa katika damu kwa aina tatu za uchunguzi. Hii ni pamoja na Uchunguzi wa VVU wa Haraka, ambayo ni uchunguzi unaoweza kutekelezwa tu nyumbani au katika Kituo cha Afya. Uchunguzi mwingine wa pili (the Western blot test and enzyme immunoassay test), zinaweza kufanyika katika kituo cha afya cha ngazi ya juu. Kulingana na urahisi wa kutumia, Uchunguzi wa VVU wa haraka hutumika kwa kawaida barani Afrika. Inahusu kuchukua kiasi kidogo cha sampuli ya damu kutoka kwenye kidole kwa kutumia chombo safi, na uchukue tone la damu ili uiweke kwenye kifaa cha kuchunguzia (Jedwali 16.1). Utajifunza jinsi ya kutekeleza uchunguzi na kusoma matokeo katika Moduli ya Magonjwa ya Ambukizi.

Picha 16.1 Sampuli ya damu inachukuliwa kwa Uchunguzi wa VVU wa Haraka. (Picha kutoka Taasisi ya Utafiti ya Afya na Lishe Afrika)

Kanuni mbalimbali ya vifaa vya kufanyia uchugnuzi wa VVU ambazo zimeendelezwa za kuchunguza damu ni sawa. Uchunguzi huu ni wa kina katika utambuzi wa maambukizi ya VVU. Zinafanya kazi kwa kugundua kingamwili (protini zinazotengenezwa na mwili ili kupambana na maambukizi) ambazo hutokea kwa damu baada ya kipindi cha utambulizi wa maambukizi ya VVU. Kipindi tambulizi ni kipindi cha muda (hadi wiki 12 au miezi 3) kati ya virusi kuingia mwilini mwa mtu na kuonekana kwa ugunduzi wa kingamwili katika damu ya mtu. Katika baadhi ya hali, mtu asiyekuwa na maambukizi ya VVU anaweza kuwa na virusi, lakini visionekane kwa sababu bado yuko katika kipindi virusi visivyotambulika. Kumchunguza mtu huyu tena baada ya miezi 3 kutoka siku ya maambukizi ya VVU matokeo yataonyesha kuwepo kwa maambukizi.

  • Sampuli kiasi cha damu ya mtu inapitishwa kwa Uchunguzi wa VVU wa Haraka kwa kutumia vifaa viwili kutoka kwa watengenezaji tofauti. Je, unaweza kueleza ni kwa nini damu hiyo imechunguzwa mara mbili kwa kutumia vifaa viwili tofauti?

  • Matokeo yataaminika zaidi ikiwa mikakati yote miwili itabainisha. Ikiwa matokeo yote mawili ni tofauti, inaonyesha kwamba uchunguzi unaweza kuwa haujafanywa vizuri na wa tatu unapaswa kufanywa kama ‘kihakikishi’

    Mwisho wa jibu

16.5 Utaratibu wa kuchunguza VVU wakati wa ujauzito

16.6 Hatua katika uchunguzi wa VVU na ushauri