16.6 Hatua katika uchunguzi wa VVU na ushauri

16.6.1 Mbinu za kushiriki na za kutoshiriki

Kuna mbinu mbili tofauti za kushauri wajawazito kuhusu umuhimu wa kuchunguzwa kwa VVU: zinajulikana kama ‘kushiriki’ na ‘kutoshiriki.’ Mbinu ya kushiriki inahusisha kushauri mwanamke kwa muda wa dakika 40 katika chumba cha kibinafsi, umjulishe kila kitu anapaswa kujua, ili akubali kuchunguzwa kwa hiari (yaani, kushiriki, au kuaminiwa na mwanamke). Hata hivyo, mwishoni mwa kipindi cha ushauri, anaweza kukataa kuchunguzwa. Mbinu ya kushiriki ulifanywa hadi mwaka wa 2006 Afrika na bado ndio inayotumiwa.

Mbinu ya kutoshiriki, kwa upande mwingine, inahusisha kumfahamisha mwanamke kwamba yuko karibu kufanyiwa uchunguzi wa VVU. Lengo kuu la mbinu ya kutoshiriki ni kuhakikisha kuwa wanawake wengi (na wanaume) wamefanyiwa uchunguzi wa maambukizi ya VVU. Tofauti kati ya kushiriki na kutoshiriki imeelezewa kwa muhtasari katika Jedwali 16.2. Hasa unavyoweza kuiona, mbinu za kutoshiriki imefaulu zaidi katika kufikia uchunguzi wa juu kuliko ilivyo kuwa kwa kushirki.

Jedwali 16.2 Kulinganisha mbinu za kushauri ya kushiriki na kutoshiriki katika uchunguzi wa VVU.
HaliKushirikiKutoshiriki
Mwongozo wa Kitaifa ya Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto20012007
KushauriKushauri kabla na baada ya uchunguzi (kabla na baada; kabla ya uchunguzi inaweza kuchukua muda mrefu hadi mteja akubali uchunguzi) Baada ya uchunguzi (baada ya matokeo ya uchunguzi isipokuwa mteja akatae kuchunguzwa au kutoshiriki)
Kiwango cha ukweli wa uchunguzi (idadi ya watu waliochunguzwa) Chini sana Juu sana
Husaidia watu kuona uchunguzi wa VVU kama ya kawaida LaNdio

Manufaa mengine ya mbinu ya kutoshiriki kwa uchunguzi wa VVU ni utaratibu wa kawaida kwa kila mtu. Kutekeleza uchunguzi wa VVU kwa kawaida husaidia kuondoa uoga wa kufanyiwa uchunguzi, kwa hivyo siku za mbeleni itakuwa kama uchunguzi wa ugonjwa mwingine wa kawaida. Taarifa kuhusu uchunguzi wa VVU unaweza kutolewa katika vikao vya vikundi, ambavyo pia husaidia; kwa mfano, unaweza kupanga mkutano wa kikundi cha wajawazito katika jamii kuyajadili masuala ya huduma inayolenga wajawazito, na utaje uchunguzi wa VVU kama sehemu ya huduma ya kawaida kwa wajawazito. Mwisho, haichukui muda mwingi wa mhudumu wa afya, kwa sababu haichukui muda mrefu kushauri kila mwanamke.

16.5.1 Kutambua maambukizi ya VVU kwa kutumia uchunguzi wa damu

16.6.2 Kushauri kina mama waliokataa kufanyiwa uchunguzi wa VVU