16.6.2 Kushauri kina mama waliokataa kufanyiwa uchunguzi wa VVU

Kuna baadhi ya mambo muhimu juu ya mbinu ya kutoshirki ambazo unahitaji kuelewa. Kwanza, mama anaweza kukataa kufanyiwa uchunguzi - yeye anaweza-kukataa. Pili, iwapo atapatikana na VVU, atapewa ushauri baada ya kuchunguzwa, mama atapewa ushauri baada ya uchunguzi. Tatu, kina mama wasioshiriki (waliokataa) watatengewa kipindi kirefu zaidi cha ushauri, ambacho huanza kwa kuwapa nafasi ya kueleza wasiwasi wao na sababu za kukataa kufanyiwa uchunguzi, kwa hivyo unaweza kushughulikia maswali yao maalum na wasiwasi.

Ili ufanikiwe kushauri kina mama waliokataa kuchunguzwa, washawishi ili wakuamini. Sisitiza kuwa utambuzi wa mapema na matibabu au tiba ya kuzuia maradhi linaboresha sana nafasi ya kuishi kwa kina mama wanalio na VVU na watoto wao. Mama akijua hali yake ya VVU haimaanishi mume wake au mwenzake ana haki ya kujua pia - ni hiari yake kuarifu hali yake ya VVU au iwe siri. Hata hivyo, akifichua hali yake, atakuwa na manufaa makubwa maana familia yake inaweza kumsaidia. Mhakikishie mama kuwa VVU si ugonjwa unaohitaji kuwa siri tena au ya aibu. Pia, si ugonjwa unaosababisha kifo, ikiwa itatambuliwa mapema na kutibiwa.

Iwapo mama ataendelea kukataa kuchunguzwa kwa VVU, ushauri zaidi unapaswa kutolewa atakapozuru kituo cha afya kwa huduma ya utunzaji katika ujauzito. Anapaswa kuhakikishiwa kuwa kukataa kwake kuchunguzwa haiathiri huduma yake ya utunzaji katika ujauzito, leba na kuzaa, baada ya kuzaa, au huduma zinazohusiana. Mshawishi achunguzwe. Usimlazimishe, lakini mjulishe kwamba ikiwa atabadili wazo lake, uchunguzi wa VVU na ushauri unaweza kutolewa katika ziara ya baadaye. Andika sababu zake za kukataa iwe kumbusho la kutoa ushauri na uchunguzi wakati ujao. Kisanduku 16.3 kinatoa muhtasari wa baadhi ya sababu za kawaida za kina mama kukataa kuchunguzwa kwa VVU.

Kisanduku 16.3 Sababu za kawaida wanawake hukataa kuchunguzwa kwa VVU

  • Uoga wa kupatikana na VVU na kupoteza matumaini.
  • Uoga wa kupatikana na VVU na kusababisha mvurugano katika ndoa na kutalakiana.
  • Uoga wa kupatikana na VVU na kutoamini wahudumu wa afya kudumisha siri ya matokeo.
  • Uoga wa kupatikana na VVU na kusababisha kuaibika na kubaguliwa na jamii.

16.6 Hatua katika uchunguzi wa VVU na ushauri

16.6.3 Miongozo ya Uchunguzi wa Haraka wa VVU