16.6.3 Miongozo ya Uchunguzi wa Haraka wa VVU

Algorithm ni seti ya miongozo inayo kuwezesha kufuata hatua kwa mipangilio ya vitendo, ikiwa na maelezo katika kila hatua kulingana na matokeo. Kielelezo 16.2 inaonyesha miongozo iliyopitishwa kwa Uchunguzi wa Haraka wa VVU Afrika.

Kielelezo 16.2 Uchunguzi wa wa Haraka wa VVU Afrika.

Kama unavyoona kutoka Kielelezo 16.2, ikiwa uchunguzi wa kwanza unaonyesha kuwepo kwa VVU, ili kuhakikisha mteja anayo VVU, kuna haja ya kufanya uchunguzi wa pili ili kuthibitisha matokeo ya uchunguzi wa kwanza.

  • Je, mwongozo katika Kielelezo 16.2 unaonyesha ni nini kinapaswa kufanyiwa ikiwa uchunguzi wa pili hauonyeshi kuwepo kwa VVU (ni kinyume na matokeo ya uchunguzi wa kwanza)?

  • Mwongozo unahitaji uchunguzi wa tatu ufanywe ili kuamua - uchunguzi huu utathibitisha matokeo ya kuwepo kwa VVU katika uchunguzi wa kwanza, au kutokuwepo katika uchunguzi wa pili.

    Mwisho wa jibu

Kufuatia hatua katika mwongozo inahakikisha kuwepo kwa VVU kumethibitishwa na vipimo viwili tofauti kabla ya matokeo kutolewa kwa mteja.

16.6.2 Kushauri kina mama waliokataa kufanyiwa uchunguzi wa VVU

16.6.4 Kujadili matokeo ya uchunguzi wa VVU: ushauri baada ya uchunguzi