16.6.4 Kujadili matokeo ya uchunguzi wa VVU: ushauri baada ya uchunguzi

Ikiwa mama amekubali, na amechunguzwa kwa VVU, unahitaji kujua jinsi ya kujadili matokeo (pamoja na mume wake) wakati wa ushauri baada ya kuchunguzwa. Kwa watu wazima, matokeo ya kuwepo kwa VVU kunamaanisha kwamba kwa hakika mtu ana maambukizi ya VVU. Kama utakavyojufunza katika Moduli za baadaye, matokeo ya kuwepo kwa VVU kwa mtoto mchanga hakumaanishi kwamba mtoto ana maambukizi. Antibodi za mama zinazokinga VVU zinaweza kuingia kwenye damu ya mtoto wakati wa leba na wa kuzaa, na ni vigumu kutambua kutokana na Uchunguzi wa Haraka wa VVU kama inatambua antibodi zake au za mtoto. Matokeo ya kutokuwepo kwa VVU kwa kawaida inamaanisha mama au mtoto hana maambukizi ya VVU.

Mama anaweza kuwa katika hatari kubwa ya maambukizi ya VVU iwapo alifanya ngono bila kinga na mtu ambaye hali yake ya VVU haijulikani, au anayejulikana kuwa na VVU, au iwapo mumewe ana mke mwingine au wenzi wengine, au mume wake anajidunga dawa za kulevya. Ikiwa matokeo ya uchunguzi wa mara ya kwanza kwa mama kama huyu yanaonyesha kutokuwepo kwa VVU, anapaswa kuchunguzwa tena baada ya miezi 3 ili kuthibitisha matokeo ya awali.

16.6.3 Miongozo ya Uchunguzi wa Haraka wa VVU

16.6.5 Ushauri baada ya kuchunguza kina mama wajawazito wanaoishi na VVU