16.6.5 Ushauri baada ya kuchunguza kina mama wajawazito wanaoishi na VVU

Unapozungumza na mama aliyepatikana na VVU, unapaswa kuwa makini sana kwa hisia zake, ambazo ni pamoja na mshtuko, hasira au kutoamini. Akiwa na uwezo wa kukusikiza, hakikisha kuwa:

 • Umuhimu wa kuzaa mtoto katika kituo cha afya cha ngazi ya juu ni kuwepo kwa dawa za kuzuia maambukizi ya virusi na pia mbinu salama za kuzaa zinatolewa, ili kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto.
 • Anaweza kupunguza hatari ya mgonjwa kwa:
  • Matumizi ya Dawa za Kupunguza Makali ya VVU zinazopendekezwa ili kuzuia magonjwa nyemelezi.
  • Kufanya ngono kwa kutumia kondomu na mwenzi wake ili kumlinda kutokana na maambukizi ya VVU, na kuhakikisha kwamba yeye hapati magonjwa mengine yoyote ya kutoka kwake ikiwa anafanya ngono bila kinga na mtu mwingine yeyote.
  • Kula chakula kingi kilicho na lishe bora, kama inavyopendekezwa kwa kina mama wote wajawazito bila kujali hali yao ya VVU (rejelea Kipindi cha 14)
  • Dumisha usafi wa kibinafsi, kama inavyopendekezwa kwa kila mtu ili kuzuia maambukizi ya bakteria, virusi, protozoa na fungi, maambukizi ya parasiti na vimelea na wadudu, na matatizo ya ngozi.
 • Jinsi ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa mtoto (kama ulivyojifunza katika kipindi hiki) ikiwa ni pamoja na njia salama ya kumlisha mtoto (utajifunza katika Moduli juu ya Udhibiti wa maradhi ya Watoto wachanga na ya Utotoni).
 • Kwamba mwenzi au mume wa mama na watoto lazima wachunguzwe kwa VVU.
 • Umuhimu wa kuzuia maambukizi ya VVU kwa watu wengine na jinsi ya kufanya hivyo.
 • Umuhimu wa rufaa kwa ufuatiliaji na maendeleo ya huduma ya afya ya VVU, mwenzake na kwa mtoto aliye katika hatari ya kuambukizwa VVU, na wanafamilia wengine.

Magonjwa nyemelezi ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria au virusi kwa watu ambao mifumo ya kingamwili yao ni dhaifu, kwa mfano kwa sababu ya VVU. Mtu aliye na afya kwa kawaida huwa na uwezo wa kupambana na maambukizi ya bakteria au virusi hivi.

16.6.4 Kujadili matokeo ya uchunguzi wa VVU: ushauri baada ya uchunguzi

16.6.6 Ushauri baada ya kuchunguza wajawazito wasio na maambukizi ya VVU