16.6.6 Ushauri baada ya kuchunguza wajawazito wasio na maambukizi ya VVU

Hata ingawa mama atakuwa na utulivu kuwa hana VVU, unapaswa kuhakikisha kuwa anaelewa:

  • Namna ya kubakia bila maambukizi ya VVU kwa kufanya ngono kwa njia salama.
  • Haja ya uchunguzi wa VVU baadaye ikiwa hatari ya maambukizi itatokea zaidi, au ikiwa uchunguzi ulifanywa mapema kabla ya antibodi za maambukizi ya VVU kujitokeza.
  • Kunyonyesha mtoto kwa kipekee (yaani, kunyonyesha tu, bila kumlisha kwa chupa au vyakula vigumu kabla ya umri wa miezi 6).
  • Iwapo ataambukizwa VVU wakati wa ujauzito au kunyonyesha, mtoto yuko katika hatari ya kuambukizwa VVU kutoka kwa Mama (rejelea Kisanduku 16.1 hapo juu).
  • Umuhimu wa upangaji uzazi madhubuti na kuacha nafasi kati ya kila mimba. (Moduli kuhusu Upangaji Uzazi itawafundisha maelezo yote ya mbinu tofauti tofauti.)

16.6.5 Ushauri baada ya kuchunguza kina mama wajawazito wanaoishi na VVU

16.6.7 Orodha ya uchunguzi na ushauri wa VVU wakati wa kipindi cha ujauzito