16.6.7 Orodha ya uchunguzi na ushauri wa VVU wakati wa kipindi cha ujauzito

Jedwali16.3 hapo chini linatoa muhtasari wa hatua zinazofuatwa katika uchunguzi na ushauri wa VVU katika kipindi cha ujauzito, wakati wanapotembelea kliniki mara ya kwanza na kila mara. Ni matumaini yetu kuwa ni ya manufaa kwako. Kumbuka pia hutapata mafunzo ya utendaji katika funzo la Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto, jambo ambalo pia litahusisha sera na taratibu wakati wa kipindi cha leba na baada ya kuzaa.

Jedwali 16.3 Orodha ya kuwashauri kina mama wajawazito kwa VVU wakati wa huduma ya ujauzito.
Uliza, ChunguzaMatokeoMatibabu na ushauri
  • Je, umewahi kufanyiwa uchunguzi wa VVU?
  • Kama ndiyo, unajua matokeo?

    (Eleza mama kwamba matokeo ni siri yake.)

  • Je mwenzake amechunguzwa?
  
  • Anayo VVU.
  • Hakikisha kwamba anamtembelea mhudumu aliye na uzoefu na kupokea taarifa muhimu kuhusu Uzuiaji wa Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto
  • Uliza kuhusu Dawa za Kupunguza Makali ya VVU na uhakikishe kuwa mama anajua wakati wa kuanza
  • Uliza jinsi atakuwa akipata dawa.
  • Uliza chaguo lake la kumlisha mtoto
  • Mshauri juu ya huduma ya ziada wakati wa ujauzito, kuzaa, na baada ya kuzaa
  • Mshauri juu ya kutumia kondomu kila mara na kwa usahihi
  • Mshauri manufaa ya kumshirikisha mwenzi wake katika uchunguzi
 

 

 
  • Hakuna matokeo ya uchunguzi wa VVU au hataki kusema.
  • Toa taarifa muhimu juu ya VVU
  • Mshauri kuhusu uchunguzi na ushauri wa kujitolea ili kujua hali ya VVU
  • Mshauri juu ya kutumia kondomu kila mara na kwa usahihi
  • Mshauri manufaa ya kumshirikisha mwenzake katika uchunguzi
  • Hana VVU
  • Toa taarifa muhimu juu ya VVU
  • Mshauri manufaa ya kuwashirikisha na kuchunguza mwenzi
  • Mshauri umuhimu wa kukaa bila kuambukizwa kwa matumizi sahihi na thabiti ya kondomu

16.6.6 Ushauri baada ya kuchunguza wajawazito wasio na maambukizi ya VVU

16.8 Huduma ya ziada kwa mama anayeishi na VVU wakati wa ujauzito