Muhtasari wa Kipindi cha 17

Katika Kipindi cha 17, ulijifunza kuwa:

  1. KTW ni kupasuka kwa tando za fetasi na kutokwa na kiowevu kutoka ukeni baada ya wiki 28 za kipindi cha ujauzito au angalau saa moja kabla ya kuanza kwa leba.
  2. KTW imeainishwa kama KTW unaotokea kabla ya muda wakati ambapo kutoka kwa kiowevu unatokea baada ya wiki 37.
  3. Wanawake walio na hali ya KTW unaoendelea kwa muda mrefu (masaa 12 au zaidi yamepita tangu kupasuka kwa tando za fetasi) wanao uwezo wa kupata maambukizi katika uterasi isipokuwa watapata matibabu ya antibiotiki ya haraka.
  4. Kipengele cha hatari kinachojulikana sana cha KTW ni pamoja na maambukizi katika mkondo wa uzazi, mlalo mbaya wa fetasi (uzazi wa kukaa au kulala vibaya kwa mtoto tumboni mwa mama), mimba ya zaidi ya watoto wawili, kiowevu kingi cha amniotiki, seviksi dhaifu, na jeraha la fumbatio.
  5. Utambuzi wa KTW unazingatia historia ya kutokwa kwa ghafula na kiowevu cha kiasi au kingi kutoka ukeni bila kuhisi uchungu. Unaweza kupata nguo za ndani zimelowa maji, kuhisi kugusika kwa sehemu za fetasi kupitia ukuta wa fumbatio lake, na kupima ukubwa wa uterasi kama ‘mdogo wa umri wa kipindi cha ujauzito’ kwa sababu fumbatio lake limepunguka.
  6. Matatizo ya kawaida yanayojulikana ya KTW ni maambukizi kwa mama na/au fetasi/mtoto mchanga, kushuka kwa kambakitovu, na ulemavu wa viungo vya fetasi.
  7. Joto jingi mwilini, mchozo ukeni ulio na harufu mbaya, ongezeko la mpwito wa ateri wa mama, ongezeko la mpigo wa moyo wa fetasi na maumivu ya sehemu ya chini ya fumbatio ni dalili ya maambukizi katika kaviti ya uterasi, ambayo yanapaswa kutibiwa haraka kwa antibiotiki.
  8. Ili kupunguza hatari za maambukizi, uchunguzi wa pelvisi kwa kutumia glavu na tarakimu unatakiwa kuepukwa kwa kina mama walio na hali ya KTW.
  9. Zalisha mtoto kisha upeane rufaa kwa hali za KTW unaotokea katika muda halisi au kabla ya muda kwa mwanamke amabaye tayari yuko katika leba inayoendelea hata ikiwa kuna uwezekano wa maambukizi au katika kesi za KTW ikiwa leba imeanza kwa kawaida na hakuna uwezekano wa maambukizi.
  10. Peana rufaa haraka iwezekanavyo kwa wanawake wote wanaokuja kwako kabla ya kuanza kwa leba au leba ya mapema, wakiwa na maambukizi yaliyodhibitishwa kwa mama au mtoto; peana rufaa kwa watoto wote wanaozaliwa kabla ya muda.
  11. Hakikisha kuwa mwanamke aliye na hali ya KTW na familia yake wanajua vyema hatari za kutotafua matibabu; washauri kuwa wakuite mara moja na waanze kuelekea katika kituo cha afya.

17.6.2 Je, ni wakati gani unapaswa kumpatia rufaa kabla ya kutekeleza uzalishaji?

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 17