Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 17

Kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki, unaweza kutathmini jinsi ulivyotimiza malengo ya somo kwa kujibu maswali yafuatayo. Andika majibu yako katika shajara yako na uyajadili na mkufunzi wako katika somo lifuatalo la Usaidizi. Unaweza kuangalia majibu yako ukitumia muhtasari wa maswali ya Kujitathmini katika mwisho wa moduli hii.

Maswali ya Kujitathmini17.1 (yanathmini Malengo ya Somo 17.1 na 17.2)

Jaza pengo lililoachwa katika Jedwali 17.1

Jedwali 17.1
Uainishaji wa KTWUmri wa Kipindi cha uajuzito
KTW unaotokea kabla ya muda
KTW unaotokea muda halisi
Muda tangu kupasuka kwa tando
KTW ya mapema
KTW inayochukuwa muda mrefu

Answer

Jedwali 17.1
Uainishaji wa KTWUmri wa Kipindi cha uajuzito
KTW unaotokea kabla ya mudaBaada ya wiki 28 na kabla ya wiki 37
KTW unaotokea muda halisiBaada ya wiki 37, ikijumuisha baada ya muda halisi (baada ya wiki 40)
Muda tangu kupasuka kwa tando
KTW ya mapemaChini ya masaa 12
KTW inayochukuwa muda mrefuZaidi ya masaa 12

Mwisho wa jibu

Maswali ya Kujitathmini 17.2 (yanathmini Malengo ya Somo 17.1, 17.3, 17.4, na 17.5)

Je, kati ya kauli zifuatazo ni gani si kweli? Kwa kila hali, eleza ni nini ambacho si sahihi.

  • A.Maambukizi katika uterasi yanaweza kusababisha KTW na pia yanaweza kuwa tatizo linalotokana na KTW.
  • B.KTW inaweza kutokea ikiwa uterasi imepanuliwa zaidi na mlalo mbaya wa fetasi, mimba ya watoto wengi, au kuna kiowevu kingi cha amniotiki.
  • C.KTW ikishirikishwa na hali ya seviksi kutokuwa na uwezo inaweza kusababisha kushuka kwa kambakitovu.
  • D.Tando za fetasi ni dhabiti kiwango cha kuwa jeraha butu la fumbatio si rahisi kusabibisha KTW.
  • E.Upungufu na ukosefu wa hewa kwa fetasi kwa mwanamke aliye katika leba ni tatizo la kawaida la KTW unaoendelea kwa muda mrefu.
  • F.Kutokwa kwa ghafula na kiowevu cheupe majimaji kutoka ukeni kwa kawaida huonekena kwa hali za KTW.

Answer

A ni sahihi. Maambukizi katika uterasi yanaweza kusababisha KTW na pia yanaweza kuwa tatizo linalotokana na KTW.

B ni sahihi. KTW unaweza kutokea ikiwa uterasi imepanuliwa zaidi na mlalo mbaya wa fetasi, mimba ya watoto wengi au kuna kiowevu kingi cha amniotiki.

C ni sahihi. KTW ikishirikishwa na hali ya seviksi kutokuwa na uwezo inaweza kusababisha kushuka kwa kambakitovu.

D si sahihi. Jeraha butu kwa fumbatio ni sababisho la kawaida la KTW.

E si sahihi. Upungufu na ukosefu wa hewa kwa fetasi (si kwa mama aliye katika leba) ni tatizo la kawaida la KTW unaoendelea kwa muda mrefu.

F si sahihi. Hali zingine za KTW hutokea bila kutokwa kwa ghafula na kiowevu cheupe majimaji kutoka ukeni, kwa hivyo lazima uchukue hesabu ya dalili za utambuzi kama vile kupungua kwa ukubwa wa fumbatio na uguse sehemu za fetasi kwa udhairi.

Mwisho wa jibu

Soma uchunguzi maalum 17.1 kisha ujibu maswali yafuatayo.

Uchunguzi maalum 17.1 Kisa cha Zufan

Familia ya Zufan wanakujulisha kuwa maji yake yalipasuka masaa 24 yaliyopita, lakini wanawasiwasi kwa sababu leba yake bado haijaanza. Wanadhani mtoto alipaswa kuzaliwa wiki iliyopita. Unapomgusa ana joto na kukosa utulivu na analalamika kuwa anahisi maumivu katika sehemu ya chini ya fumbatio lake.

Maswali ya Kujitathmini 17.3 (yanathmini Malengo ya Somo 17.1, 17.2, 17.5 na 17.6

  • a.Je, utaainisha vipi hali ya Zufan ya KTW?
  • b.Je, anazo dalili za matatizo yoyote?
  • c.Je, kunalo jambo lolote ungelifanya ili kuzuia hali yake isi zidi?
  • d.Je, ni hatua gani ya haraka unayopaswa kuchukua?

Answer

  • a.Hali ya Zufan inafaa kuainishwa kama KTW unaoendelea kwa muda baada ya kutokea, kwa sababu umri wa kipindi cha ujauzito tayari imepita wiki 40 na tando zake zilipasuka zaidi ya masaa 12 yaliyopita.
  • b.Anazo dalili mbili zilizodhihirika za maambukizi ya fumbatio: joto jingi mwilini na maumivu katika sehemu ya chini ya fumbatio.
  • c.Ungelizuia hali yake kuwa isi zidi ikiwa ulikuwa umemshauri Zufan na familia yake kwa udhairi zaidi kuhusu hatari za kutotafuta matibabu baada ya kupasuka kwaTando.
  • d.Unapaswa kumpa rufaa haraka kwenye hospitali iliyoko karibu au kituo cha afya kilicho na vifaa vya kufanyia upasuaji; pia atahitaji antibiotiki haraka za kutibu maambukizi.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 17