17.1 Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati (KTW)

KTW inafafanuliwa kama kutokwa na kiowevu cha amniotiki kutoka mfuko wa amniotiki ambapo mtoto huogelea; kiowevu hupitia kwenye tando za fetasi zilizopasuka, hii hutokea baada ya wiki 28 za kipindi cha ujauzito na angalau saa 1 kabla ya kuanza kwa leba. KTW unaweza kutokea kabla au baada ya wiki 40 ya kipindi cha ujauzito kwa hivyo ‘kabla ya wakati ‘haimaanishi kuwa umri wa fetasi katika kipindi cha ujauzito haujakamilika.

Kabla ya wakati inamaanisha kupasuka kwa tando za fetasi kabla ya leba kuanza. KTW ni tatizo kwa sababu sio kawaida na huhusishwa na matatizo mengi (zitakazoelezwa baadaye katika Kipindi hiki.) Katika leba ya kawaida, tando za fetasi hupasuka baada ya leba kuendelea kwa muda, wakati kichwa cha fetasi kimeshirikishwa na kupanuka kwa seviksi bila tatizo kwa wanawake waliopo katika leba. (Utajifunza kwa kina kuhusu maendeleo ya leba katika Moduli inayofuata, (Utunzaji wa leba na kuzaa)

Unapaswa kufahamu kuwa watu wengi barani Afrika hawajui kwamba KTW ni shida. Bali hudhania kutokwa na kiowevu ni dalili nzuri ya leba inayokuja. Kama utakavyoelewa baadaye katika kipindi hiki, matatizo mengi ya hatari yanaweza kutokea kutokana na KTW. Kwa hivyo, unapaswa kumshauri mwanamke, mume wake na famillia yake kuhusu hatua wanazopaswa kuchukua tando zake zikipasuka na kiowevu kutoka ukeni kabla ya leba kuanza.Wajulishe hatari za kukaa nyumbani baada ya kupasuka kwa tando. Tunaanza kwa kueleza jinsi unavyoainisha hali za KTW, zinazokusaidia kuzishughulikia hali hizo.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 17

17.2 Uainishaji wa Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati (KTW)