17.2 Uainishaji wa Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati (KTW)

KTW huainishwa kulingana na umri wa kipindi cha ujauzito wakati tando hupasuka na muda kati ya kupasuka kwa tando la fetasi na mwanzo wa leba.

KT W unaotokea kabla ya muda hufanyika baada ya wiki 28 za umri wa kipindi cha ujauzito na kabla ya wiki 37.

KTW unaotokea katika muda halisi hufanyika baada ya wiki 37 zilizokamilika za umri wa kipindi cha ujauzito zikiwemo hali za baada ya kipindi zinazotokea baada ya wiki 40.

Kupasuka kwa tando kabla ya muda na katika muda halisi unaweza kutenganishwa zaidi:

  • KTW unaotokea mapema (masaa 12 hayajapita tangu kupasuka kwa tando za fetasi.)
  • KTW unaoendelea kwa muda mrefu (masaa 12 au zaidi yamepita tangu kupasuka kwa tando ya fetasi.)

Sababu kuu za kuainisha KTW katika muda halisi, kabla ya muda, mapema na unaoendelea kwa muda mrefu ni kwa sababu ya kutekeleza uamuzi wa kudhibiti. Jinsi kunavyotokea mapema (KTW unaotokea kabla ya muda.) na jinsi muda ulivyo mrefu kati ya kupasuka kwa tando za fetasi na kuanza kwa leba, ndivyo kulivyo na uwezekano wa matatizo mengi zaidi. Tutaeleza hatua unazopaswa kuchukua ili kudhibiti hali za KTW katika kitengo cha 17.6 cha kipindi hiki. Kwanza tujadili vipengele vya hatari vya KTW na matatizo yanayoweza kutokea kwa mama na fetasi.

17.1 Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati (KTW)

17.3 Vipengele vya hatari ya KTW