17.3.1 Maambukizi yanaweza kusababisha KTW

Bakteria inaweza kusababisha maambukizi katika mkondo wa chini wa viungo vya uzazi (maambukizi ya seviksi au ukuta wa uke) zinaweza kupanda juu kupitia seviksi na kuambukiza tando za fetasi. Hili linaweza kudhoofisha tando hadi zipasuke.

Kisanduku 17.1linatoa muhtasari wa dalili za kutambua maambukizi ya KTW kwa mwanamke.

Kisanduku 17.1 Thibitisho la maambukizi kwa mwanamke aliye na shida ya KTW.

  • Joto jingi: mwanamke anaweza kulalamika kuwa anahisi joto au unaweza kunakili halijoto yake ya sentigredi 38 au zaidi.
  • Mchozo kutoka ukeni unaoweza kuwa na harufu mbaya na rangi inaweza kubadilika kutoka hali ya majimaji na kuwa yenye mawingu.
  • Anaweza kuwa na ongezeko la mpigo wa moyo (zaidi ya mipigo 100 kwa dakika)
  • Mpigo wa moyo wa fetasi unaweza kuongezeka hadi mipigo 160 kwa dakika au zaidi.
  • Anaweza kuhisi maumivu katika sehemu ya chini ya fumbatio lake, hasa linapoguswa.

17.3 Vipengele vya hatari ya KTW

17.3.2 Mlalo mbaya wa fetasi