17.3.4 Seviksi dhaifu

Bila mikazo ya uterasi, seviksi inaweza kupanuka mapema katika kipindi cha ujauzito na hii inaweza kuwa sababisho la utokaji wa mimba (kuharibika kwa mimba). Seviksi inaweza kupanuka hata baadaye katika kipindi cha ujauzito kabla ya kuanza kwa leba. Sehemu ya tando za fetasi zitaruhusiwa kupita, wakati seviksi inaendelea kupanuka. Kwa hivyo, tando zinaweza kupasuka kwa urahisi na kufanya kiowevu cha amniotiki kutoka.

17.3.3 Ujauzito ya watoto wengi na kiowevu kingi cha amniotiki

17.3.5 Jeraha la fumbatio