17.4 Utambuzi wa KTW

Wakati kuna mpasuko katika tando za fetasi, mwanamke hugundua utokaji wa kiowevu ambacho huwa ni kingi sana na majimaji, kutoka ukeni bila uchungu wowote. Hata hivyo, wakati kiowevu cha amniotiki ni kidogo, kiowevu kinachotoka kinaweza kulowesha nguo za ndani, na utakuwa na uhakika wa kutekeleza utambuzi wa KTW kutokana na malalamishi ya mwanamke.

Mama anaweza kuwa na wasiwasi, lakini hana uhakika kama utokaji wa kiowevu ni kawaida au sio kawaida. Ni kawaida kwa mchozo kutoka ukeni na kuongezeka kwa kiasi kidogo mwanamke anapokaribia mwisho wa ujauzito, na hili linaweza kutatanishwa na utokaji wa kiowevu cha amniotiki. Kwa hivyo unapaswa kumpa rufaa mwanamke yeyote anayelalamika kuhusu utokaji wa mchozo ukeni kwa utathmini zaidi katika kituo cha afya cha juu, iwapo mwanamke anaonyesha ishara za KTW.

Kisanduku 17.1 linafupisha dalili za ugonjwa ambayo unaweza kukusaidia kutekeleza utambuzi wa KTW.

Kisanduku 17.1 Dalili za ugonjwa ya KTW

  • Mwanamke hulalamika kuhusu utokaji wa kiowevu kutoka ukeni (kidogo sana au kingi zaidi.)
  • Aligundua kupungua kwa ukubwa wa fumbatio lake baada ya kutokwa na kiowevu.
  • Unaona kiowevu cha majimaji kinachotoka ukeni, au nguo za ndani zimelowa kiowevu cha majimaji.
  • Unapopima umbali kati ya simfisis ya mfupa wa kinena na urefu wa fandasi (kama ilivyoelezwa katika Kipindi cha 9), unapata kuwa mtoto ni mdogo katika kipindi cha ujauzito. (Fahamu ya kwamba kuwa ‘udogo wa kipindi cha ujauzito’ inaweza pia kusababishwa na uhaba wa kiwango cha kiowevu cha amniotiki na tando zisizoharibika, kizuio cha uvimbe wa ndani ya uterasi, na tarehe ambayo si sahihi kwa umri wa kipindi cha ujauzito uliyotajwa.)
  • Katika KTW, kiowevu cha amniotiki kilichobakia kwenye mfuko kitakuwa kidogo. Kwa hivyo unaweza kuhisi (chunguza kwa kugusagusa) sehemu za fetasi kwa urahisi kupitia fumbatio la mama.
  • Hata kama si dhairi, mwanamke anaweza kuwa na harufu mbaya inayosababishwa na mchozo ukeni, na kuwa na joto jingi mwilini (tazama Kisanduku 17.1 hapo juu); dalili hizi zinaashiria maambukizi ambayo tayari yamedhibitishwa, yanaweza kuwa sababisho la KTW.
  • Unaweza kumpatia pedi iliyokauka au Goth na uiangalie baada ya masaa fulani kama ni majimaji au bado ni kavu. Fahamu kuwa ikikauka haimaanishi kuwa hakuna uwezekano wa KTW.

17.3.5 Jeraha la fumbatio

17.5 Matatizo ya KTW