17.5.1 Maambukizi baada ya KTW
Kupasuka kwa tando za fetasi kabla ya wakati huruhusu bakteria kuingia katika kaviti ya uterasi, kama ilivyoelezwa hapo awali, Huzaana haraka katika maeneo yaliyovuguvugu, majimaji na kutokana na hayo, mama pamoja na fetasi wanaweza kupata maambukizi yanayotisha maisha.Yanaweza pia kuendelea hata baada ya kuzaa kama uterini au maambukizi yaliyoeneaa kwa upana kwa mama, na kusababisha nimonia, sepsis (maambukizi ya damu) au meninjitisi (maambukizi ya ubongo) katika mtoto mchanga.
Maambukizi ni mojawapo ya matatizo ya KTW yanayohofiwa sana kwa sababu, yasipotibiwa haraka, yanaweza kusababisha kifo kwa mama na fetasi au mtoto mchanga. Lakini habari njema ni kuwa ukitibu haraka kwa kutumia antibiotiki mara nyingi hufaulu.
Lazima ifahamike kuwa hali za KTW zinazoendelea kwa muda mrefu isipotibiwa na antibiotiki ya kukinga, zinaweza kusababisha maambukizi ya uterasi.
KTW inayochukua muda mrefu inaweza kusababisha maambukizi kwa nini?
Masaa 12 yamepita tangu tando za fetasi zipasuke, kwa hivyo bakteria yoyote inayoingia katika uterasi inayo muda wa kutosha kuzaana na kujishikilia.
Mwisho wa jibu
17.5 Matatizo ya KTW