17.5.2 Kushuka kwa kambakitovu

Mchoro 17.1 Kushuka kwa kambakitovu ni tatizo la hatari ya KTW.

Kushuka kwa kitovu ni mojawapo ya matatizo ya KTW zinazoweza kusababisha kifo cha mtoto. (Jina ‘prolapse’ linamaanisha ‘kusukuma kutoka mahali panapokaa’.) Tando zinapopasuka, kambakitovu inaweza kusukumwa kuelekea chini na mkurupuko wa kiowevu cha amniotiki na kuanguka ikielekea kwenye uke. Inaweza kusukumwa mbele ya mtoto mpaka kwenye seviksi (tazama Mchoro 17.1) kupitia mpasuko katika tando. Katika hali hii kambakitovu iliyoshuka hubanwa kwa urahisi, na hivyo kuzuia usafirishaji wa damu kwa fetasi na hili linaweza kusababisha kifo cha ghafula ya fetasi.

17.5.1 Maambukizi baada ya KTW

17.5.3 Upungufu na ukosefu wa hewa kwa fetasi