17.5.6 Ulemavu wa viungo vya fetasi
Wakati mwingine leba haianzi baada ya KTW. Hali huwa ni hatari na waweza kupata maambukizi na ulemavu wa fetasi, ikiwa itatokea mapema wakati wa ujauzito na ujauzito kuendelea kwa muda mrefu baada ya tando kupasuka.
Pasipo na kiowevu cha amniotiki cha kuifanya fetasi ‘kuelea’, kuta zenye misuli ya uterasi huzingira fetasi kwa karibu na kuibana. Mifupa isiyokomaa ya fetasi tayari haina nguvu za kutosha za kukinga shinikizo, na kuna uwezekano wa kupata ulemavu wa miguu, nyayo, mikono au viganja ikiwa ujauzito utaendelea katika hali hii kwa muda wa zaidi ya wiki 3.
17.5 Leba inayoanza kabla ya muda