19.1.4 Muhtasari wa matatizo ya mama na fetasi ya priklampsia kali
| Matatizo kwa mama | Matatizo kwa fetasi |
|---|---|
| Eklampsia | Kuachia kwa plasenta |
| Kutokwa na damu ndani ya kichwa (kutoka damu ndani ya fuvu la kichwa) | Asifiksia ya ndani ya uterasi (ukosefu mkubwa wa oksijeni kwenye uterasi) |
| Anemia | Uzuiaji wa ukuaji ndani ya uterasi |
| Idadi ya chini ya pleteleti, ugandaji duni wa damu, na hatari ya kutokwa na damu | Kuzaa kabla ya muda kamili kutimia |
| Figo kutofanya kazi | Fetasi kufariki ndani ya uterasi |
| Ini kutofanya kazi, au hata kuraruka kwa ini | Ugumu katika kupumua baada ya kuzaliwa (asifiksia ya mapema ya mtoto mchanga) |
| Kiowevu kwenye mapafu (edema ya mapafu) | Upunguani |
| Moyo kutofanya kazi | |
| Upofu kamilifu wa muda |
Back to previous pagePrevious
19.1.3 Matatizo yanayotokea sana ya priklampsia kali kwa mama
