19.2.1 Uainishaji wa prikilampsia
Priklampsia ndiyo aina ya magonjwa ya kihipatensheni inayotokea sana katika ujauzito na iliyoangaziwa sana katika majadiliano ya sehemu hii (tazama Jedwali 19.2 ). Hutokea katika nusu ya pili ya ujauzito (baada ya majuma 20 ya ujauzito, lakini hutokea sana baada ya majuma 28). Kuwepo kwa protini katika mkojo wa mwanamke (protinuria) ni ishara ya hatari. Protinuria nyingi hufafanuliwa kama kipimo chanya cha mkojo cha dipstick chenye matokeo zaidi ya au sawa na +2 kwenye kipimo cha dipstick hizo.
Aina | Shinikizo la juu la damu (lililopimwa mara mbili, saa sita kati ya vipimo hivi) | Protinuria | Dalili za ukali |
---|---|---|---|
Hipatensheni yaujauzito (hutokea katika ujauzito na kuisha baadaye) | Zaidi ya kipimo cha 140/90 mmHg | Hakuna protinuria nyingi | Hakuna |
Priklampsia ndogo | Kati ya 140/90 mmHg na 160/110 mmHg | Hakuna protinuria nyingi | Hakuna |
Priklampsia kali | Zaidi ya au sawa na 160/110 mmHg | Protinuria inayoonekana iwepo au isiwepo (matokeo ya kipimo cha dipstick zaidi ya au sawa na +2) | Maumivu ya kichwa, kiwaa, maumivu ya epigasriamu, kupungua kwa mkojo, kupungua au kutokuweko kwa kucheza kwa mtoto |
Priklampsia zaidi juu ya iliyokuwepo awali | Juu kuliko kabla ya ujauzito kwa mwanamke aliye na hipatensheni sugu | Protinuria inayoonekana nyingi zaidi au inayozidi | Kuwe au kusiwe na dalili za ukali |
19.2 Uainishaji wa hipatensheni katika ujauzito