20.1 Je, kuvuja damu mapema katika ujauzito ni nini?

Kuvuja damu kabla ya wiki 28 za ujauzito hudhaniwa kuwa ni kuvuja damu mapema katika ujauzito. Ikitokea baada ya wiki 28, huitwa utokaji wa damu wa baadaye katika ujauzito. Mkato huu wa wiki 28 umezingatia uwezekano wa kuishi ikiwa mtoto atazaliwa kabla ya tarehe iliyotarajiwa katika wiki 28. Matumaini ya kuishi kabla ya wiki 28 ni madogo sana katika nchi nyingi zinazoendelea maana kuna upungufu wa vifaa vya afya vya utunzaji maalum kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. Siku hizi nchi zingine zimepunguza mkato huu hadi wiki 20 kwa sababu ya utunzaji ulioimarishwa na teknolojia inayotolewa na mfumo wao wa afya.

Visababishi vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito ni utoaji wa mimba, kutoka kwa mimba mapema kwa sababu ya kufa kwa fetasi. Visababishi vingine viwili vya kawaida ni mimba iliyotungwa nje ya uterasi (Wakati fetasi hujitia na kukua nje ya uterasi), na mimba isiyokuwa ya kawaida (wakati uvimbe unakua katika uterasi badala ya fetasi). Tutarejelea matatizo haya tukikaribia mwisho wa kipindi hiki, lakini lengo letu kuu ni uavyaji mimba.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 20

20.2 Uavyaji mimba