20.2 Uavyaji mimba

20.2.1 Mimba kutoka pekee yake

Mimba kutoka pekee yake (kuharibika kwa mimba) hutokea kwa kawaida katika 15% ya mimba, wakati mwingine hutokea mapema sana kiasi cha kuwa mwanamke hawezi kufahamu kuwa alikuwa mjamzito. Hata hivyo, kuharibika kwa mimba pekee yake wakati mwingine inaweza kusababisha uvujaji wa damu nyingi na kuhatarisha maisha ya mwanamke. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa, jeraha, vurugu, malaria na mafadhaiko yanaweza kufanya mimba kutoka mapema. Wakati mwingine mimba huharibika kwa sababu mwanamke amekuwa karibu na sumu au kemikali zilizo na toksini. Si rahisi kujua kila wakati kinachosababisha uharibikaji wa mimba, lakini visababishi vingine vya kuharibika kwa mimba vinaweza kukingwa. Kuharibika kwa mimba wakati mwingine unaweza kukingwa kwa kutibu wanawake kutokana na maradhi na maambukizi na kuwasaidia kuepukana na sumu ya kemikali na vurugu. Lakini wanawake wengine huwa na uharibikaji wa mimba mmoja baada ya nyingine, na huweza kushindwa kujua ni kwa nini.

Wanawake walio na historia ya uharibikaji wa mimba unaojirudia wanapaswa kutibiwa katika kituo cha afya kilicho na huduma za kipekee ili kutafuta sababisho na kuwasaidia kubeba mimba hadi mwisho wa ujauzito.

20.1 Je, kuvuja damu mapema katika ujauzito ni nini?

20.2.2 Utoaji mimba wa kupanga