20.2.2 Utoaji mimba wa kupanga

Mimba zisizopangwa na zisizotarajiwa, hasa katika wasichana wanaobalehe, zinaweza kusababisha mwanamke kukimbilia utoaji mimba wa kupanga (kukomesha ujauzito kimakusudi). Katika hali fulani kwa nchi zingine, utoaji mimba ulioruhusiwa unaweza kutekelezwa kwa usalama katika kituo cha afya na mhudumu wa kiafya aliyehitimu. Utaratibu huu kwa kawaida hauhatarishi ujauzito wa siku sijazo wa mwanamke. Msimamo wa kisheria na njia zinazokubalika za kutoa mimba kwa usalama zimeelezwa katika kitengo 20.2.4 cha kipindi hiki.

Mchoro 20.1 Utoaji mimba usio salama unaweza kusababisha kuvuja damu nyingi, maambukizi hatari, ukosefu kuzaa tena au hata kifo.

Utoaji mimba usiokuwa salama ni mimba unaotolewa na mwanamke mwenyewe au na mtu asiye na ujuzi katika mazingira safi chafu (Mchoro 20.1).

Mwanamke aliyekuwa mgonjwa, aliyejeruhiwa, au aliyevuja damu nyingi baada ya kutoa mimba anaweza kuwa na kovu katika uterasi zinazoweza kusababisha matatizo katika ujauzito wa siku sijazo. Kifo kutokana na utoaji mimba usiokuwa salama ni mojawapo ya visababishi vya vifo na maradhi kwa kina mama ulimwenguni vinavyoongoza hasa katika nchi zinazokuwa. Ni sababisho kuu la vifo kwa kina mama na linahitaji kushughulikiwa ili kupunguza vifo vingi kwa kina mama nchini.

20.2.3 Uainishaji wa dalili za utoaji mimba