20.2.3 Uainishaji wa dalili za utoaji mimba

Matokeo ya mimba kutoka pekee yake au utoaji wa mimba uliopangwa yameainishwa kwa kuzingatia mawasilisho ya kliniki, kama ilivyoamuliwa na mhuduma wa afya. Ni muhimu kujua aina tofauti, kwa sababu utakavyomtibu mwanamke hutegemea na uainishaji wa kliniki.

Utoaji mimba uliokamilika

Utoaji mimba uliokamilika inamaanisha kuwa sehemu zote za fetasi na plasenta zimetolewa kupitia uke; hakuna kilichobaki katika uterasi na seviksi imefungika. Hakuna utaratibu wa matibabu wa kutoa kila kitu (tupu) kwa kawaida huhitajika. Baada ya utoaji mimba uliokamilika ambao ulitekelezwa kwa usalama mwanamke anaweza kuhisi maumivu madogo katika fumbatio lake, na uvujaji damu kutoka ukeni unapaswa kuwa kama hedhi ya kawaida.

Ikiwa uvujaji damu ni karibu wastani, na kunazo tishu za fetasi zinazotoka kupitia mdomo wa uterasi, unaweza kuzitoa kwa upole kwa kidole kilichofishwa vimelea kilichovalishwa glavu. Usijaribu kufanya hadi ukamilishe mafunzo yako ya kiutendaji katika ustadi huu. Mpe mwanamke µg400 (mikrogramu) ya misoprostol kwa mdomo kabla ya kumpa rufaa kwenye kituo cha afya kilichoko karibu.

Utoaji mimba usiokamilika

Utoaji mimba usiokamilika ni wakati sehemu ya tishu za fetasi au plasenta zingali kwenye uterasi na seviksi imefunguka. Ukiacha utoaji mimba usiokamilika bila matibabu kwa muda, kunao ongezeko la hatari kuwa itatatizwa na maambukizi na hili linaweza kuwa tisho la maisha ya mwanamke.

Utakapo hudhuria mafunzo ya kiutendaji yanayohusiana na kipindi hiki utaona jinsi tishu iliyobaki kwa uterasi inaweza kutolewa kwa vifaa, kwa kutumia mbinu inayoitwa uhamishaji na kuretaji. Pia utajifunza jinsi ya kumpatia mwanamke dawa kwa njia ya mdomo na kumdunga sindano katika misuli ya paja au matako (udungaji wa sindano ndani ya musuli, au IM) ili kusaidia katika njia hii.

Utoaji mimba ulio hatari

Mimba ikitatizwa na uvujaji damu kutoka ukeni, lakini seviksi imefungika inaweza kuashiria utoaji wa mimba ulio hatari. Kuna uwezekano ujauzito unaweza kuendelea kwa kawaida, ikiwa fetasi inaonyesha dalili za kuishi.

Ikiwa utashuku utoaji wa mimba ni hatari, rufaa mwanamke kwenye kituo cha afya kilichoko karibu, wanapoweza kutunza mimba.

Utoaji mimba usioepukika

Utoaji mimba usioepukika ni wakati fetasi iko kwenye uterasi, lakini ujauzito haswa utafika mwisho fetasi ikitolewa. Mara nyingi mwanamke huwa na maumivu katika sehemu ya chini ya fumbatio na badiliko la seviksi linaloitwa ufutaji, wakati seviksi imejivuta nyuma na kuwa nyembamba; halafu seviksi inaanza kupanuka na kufunguka kama wakati wa leba ya kawaida ya kipindi kilichokamilika. (Utajifunza kuhusu ufutaji na kupanuka kwa seviksi katika, Moduli inayofuata ya Utunzaji wa leba na kuzaa. Vilivyoko kwenye uterasi vitatoka nje pekee yake lakini ikiwa hili halitafanyika, utafunzwa umpatie mwanamke µg400 (mikrogramu) za misoprostol kwa mdomo, ikirudiwa mara moja baada ya masaa 4 ikilazimu. Usijaribu kufanya hivi hadi ukamilishe mafunzo yako katika ustadi huu.

Utoaji mimba usiofanikiwa

Wakati fetasi yote iko kwenye uterasi, lakini haina ishara zozote za kuishi na seviksi imefungika kabisa, hali hii huitwa utoaji mimba usiofanikiwa. Fetasi iliyokufa huenda ikabaki kwenye uterasi kwa muda labda itolewe katika kituo cha afya cha kipekee.

Kutoa fetasi iliyokufa baada ya utokaji wa mimba usiofanikiwa kwa kawaida huhitaji huduma za kipekee za hospitali bora, kwa hivyo unapaswa kufanya kila juhudi za kumpa mwanamke rufaa kwenye kituo cha afya cha juu zaidi kilicho karibu.

20.2.2 Utoaji mimba wa kupanga

20.2.4 Mtazamo wa kisheria kuhusu utoaji mimba