20.2.4 Mtazamo wa kisheria kuhusu utoaji mimba

Katika nchi kadhaa, utoaji mimba umekubaliwa tu ili kuokoa maisha ya mwanamke, kulinda afya yake, na katika visa vya ubakaji. Katika nchi hizo, utoaji mimba sio makosa wakati inapofanywa ili kuokoa maisha ya mwanamke au afya yake; katika kesi za ubakaji, kujamiiana kwa maharimu au kuharibika sana kwa fetasi; au wakati mwanamke mjamzito hukosa uwezo wa kumtunza mtoto wake kwa sababu ya uchanga wake wa umri au upungufu wake wa kimwili au afya yake ya kiakili.

  • Semira amekueleza kuwa ni mjamzito. Yuko katika afya bora. Hana mtu aliye imara na hataki mtoto. Je, sheria inamruhusu kutoa mimba? Eleza ni kwa nini ndio au la.

  • Semira hastahili kutoa mimba isipokuwa kama alikuwa amebakwa, wana uhusiano wa kifamilia na baba yake mtoto (kujamiiana kwa maharimu), au hana uwezo wa kumtunza mtoto kwa sababu ya ugonjwa mbaya wa kiakili au kimwili.

    Mwisho wa jibu

20.2.3 Uainishaji wa dalili za utoaji mimba

20.2.5 Njia za kutekeleza uavyaji mimba