20.3.2 Ujumbe muhimu kwa wanawake baada ya mimba kutoka pekee yake au uliopangwa

Kutoa usaidizi wa kihisia

Mchoro 20.2 Ujauzito ukifika mwisho mapema, msaidie mwanamke kupata nafuu ya kihisia.

Ujauzito unapofika mwisho mapema, mwanamke anaweza kuwa na hofu, huzuni, au mfadhaiko au anaweza kuhisi mwenye hatia au kuaibika. Wanawake wengi, hasa ambao hawajaolewa, huhisi kuwa ni lazima wafiche uharibikaji wa mimba au utoaji wa mimba uliopangwa kwa sababu ya fikira dhidi ya ngono, kupanga uzazi au utoaji mimba katika jamii zao. Kama mhudumu wa afya wa karibu zaidi na aliyeaminika sana, unao wajibu muhimu wa kutekeleza katika kumhurumia mwanamke na kumpa usaidizi wa kihisia (Mchoro 20.2).

Iwapo mimba ilitoka pekee yake, mjulishe kuwa hii hutokea mara nyingi kwa sababu ya ugonjwa wa mama au matatizo ya fetasi inayokua. Mhakikishie kuwa kuna uwezekano wa kuwa na ujauzito nzuri unaofuata, isipokuwa kama kumekuwa na maambukizi kwa uterasi, au chanzo cha kuharibika kwa mimba hakijatambuliwa na inayoathari kwa mimba inayofuata. Ikiwa mwanamke anahitaji mtoto mwingine, mshawishi acheleweshe ujauzito unaofuata mpaka apone vizuri kutokana na uharibikaji au utokaji wa mimba.

Kuvunja mfuatano wa mimba zisizohitajika

Wajibu mwingine ni kutoa huduma ya upangaji uzazi kwa wale wanaohitaji, pamoja na kuvunja mfuatano wa mimba zisizohitajika na utoaji wa mimba zilizopangwa. Ikiwa ujauzito hauhitajiki baada ya kutoa mimba na hakuna matatizo ya kudumu zinazohitaji matibabu zaidi, mwanamke anapaswa kupokea ushauri wa kutosha na usaidizi wa kuchagua njia inayofaa zaidi ya kupanga uzazi ambayo inaweza kutekelezwa moja kwa moja. Kitengo 20.5 cha kipindi hiki kinaeleza utangulizi mfupi wa upangaji uzazi baada ya kutoa mimba.

Utunzaji baada ya kutoa mimba salama

Baada ya mimba kutoka pekee yake au iliyopangwa kwa usalama, Mjulishe mwanamke atarajie kuhisi maumivu madogo au spazimu katika sehemu ya chini ya fumbatio lake, na uvujaji wa damu kidogo kutoka ukeni – sio zaidi ya damu ya hedhi ya kawaida. Mjulishe jinsi yeye na familia yake wanaweza kumtunza kwa siku chache (Mchoro 20.1).

Kisanduku 20.1 Utunzaji baada ya mimba kutolewa salama

Utunzaji bora baada ya mimba kutoka pekee yake au mimba uliopangwa unaweza kuzuia maambukizi na kusaidia mwili wa mwanamke kupona haraka. anapaswa:

  • Kunywa viowevu vingi na kula vyakula vilivyo na virutubishi.
  • Kupumzika mara kwa mara na kuepukana na kazi nzito kwa wiki.
  • Kuoga kila siku, lakini hapaswi kusafisha kaviti au kuketi kwa bafu au beseni ya maji mpaka siku chache baada ya uvujaji damu kukoma.
  • Kutumia nguo safi au pedi kushika damu yoyote, na kubadilisha pedi mara kwa mara.
  • Kutotia kitu chochote ndani ya uke, na kuepukana na ngono kwa angalau siku chache baada ya uvujaji damu kukoma.

Mwambie akujulishe mara moja au atafute usaidizi kutoka kwenye kituo cha afya cha juu ikiwa anazo ishara zozote za onyo zilizoorodheshwa katika kitengo kifuatacho.

20.3.1 Malengo ya huduma baada ya kutoa mimba

20.3.3 Utunzaji wa kufuatilia baada ya kutoa mimba