20.3.3 Utunzaji wa kufuatilia baada ya kutoa mimba

Uzuiaji wa magonjwa yanayohusishwa na utoaji wa mimba na vifo hutegemea upatikanaji wa utunzaji wa mwanamke baada ya kutoa mimba katika mfumo wote wa utunzaji afya. Kama ni habari ya afya na elimu, uimarishaji wa dalili na utoaji rufaa wakati unaofaa, njia salama za kutoa mimba, au utunzaji wa kipekee kwa matatizo makali, angalau baadhi ya sehemu za utunzaji baada ya utoaji wa mimba unapaswa kupatikana katika kila mahali pa kutoa huduma ya uzalishaji katika mfumo wa utunzaji afya, pamoja na vituo vya afya. Ikiwa mwanamke alikuwa na uharibikaji wa mimba au utoaji mimba wa kupanga uliosalama katika kituo cha afya, anao uwezekano mdogo wa kupata maambukizi hatari au jerahi kuliko mwanamke ambaye alifanyiwa utoaji wa mimba kwa njia haramu na mtu aliyetumia vifaa visivyo salama.

Utunzaji wa dharura baada ya kutoa mimba inamaanisha hatua unazopaswa kuchukua ikiwa matatizo yaliyo katika Kisanduku 20.2 yatatokea kutokana na utoaji wa mimba.

Kisanduku 20.2 Matatizo baada ya kutoa mimba kwa njia isiyosalama

Tatizo kuu la hatari zaidi ni kifo. Imekadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya vifo vya kina mama ni kwa sababu ya utoaji wa mimba kwa njia isiyo salama. Kwa kila mwanamke anayekufa, imekadiriwa kuwa wanawake wengine 16 hadi 33 huwa na tatizo baada ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama, pamoja na:

 • Hemoreji (kutokwa na damu nyingi)
 • Maambukizi katika kaviti ya pelvisi, au katika mkondo wa damu. (kwa mfano, pepopunda)
 • Kutoboka kwa uterasi (kushona mraruko wa kuta za uterasi kwa kifaa kilicho na ncha kali.
 • Jerahi lililokaribu na ogani katika kaviti ya pelvisi (kwa mfano, uke, kibofu cha mkojo, rektamu na utumbo)
 • Sumu kutokana na dozi ya dawa iliyozidi kipimo chake au mitishamba inayotumiwa kutekeleza utoaji mimba wa kupanga.

Hapo baadaye, mwanamke anaweza kuugua kutokana na maumivu ya pelvisi yanayoendelea kwa muda mrefu (yanayojirudia), hasa wakati wa hedhi, mimba kutoka pekee yake unaojirudia au utasa.

Ikiwa mwanamke anayo ishara yoyote kati ya hizi baada ya kutoa mimba, mwelekeze kwenye kituo cha afya kilichoko karibu au hospitali

Unapaswa kuchunguza afya ya mwanamke, mpigo wa mshipa, halijoto, shinikizo la damu mara kwa mara baada ya kutoa mimba na mwulize na uwe makini ikiwa anayo ishara na dalili zinazofuata:

 • Maumivu makali ya spazimu katika sehemu ya chini ya fumbatio.
 • Sehemu ya chini ya fumbatio lililovimba au lililongumu bila sauti au mibubujiko ndani.
 • Uvujaji wa damu nzito, donge kubwa la damu au kuvuja damu kwa zaidi ya wiki 2
 • Harufu mbaya kutoka ukeni.
 • Joto jingi mwilini: halijoto ya sentigredi 38 au iliyo juu.
 • Mpigo wa kasi wa mshipa: zaidi ya mipigo 100 kwa dakika.
 • Kuhisi kichefuchefu sana, kupoteza fahamu, au kuwa na kizunguzungu.
 • Shinikizo la damu lililochini au linaloshuka, chini ya kiwango cha kawaida ya mmHg 120/70.

Ikiwa kutatokea uvujaji wa damu nzito, unaweza kushindwa kuona kama damu inavuja kwenye fumbatio lake kutoka kwenye jerahi au ogani nyingine ya ndani, ambalo linaweza kutendeka baada ya kutoa mimba. Upotezaji wa damu nyingi unasababisha hali inayoitwa mshtuko (Kisanduku 20.3).

Kisanduku 20.3 Ishara za mshtuko

Mwanamke aliye na mshtuko ataonekena mwenye rangi ya buluu hafifu na kutokwa na jasho, na mpigo wa kasi wa mshipa (juu ya mipigo 100 kwa kila dakika), upumuaji wa kasi, shinikizo la damu lililo chini au linaloshuka (shinikizo la diastoli – nambari ya chini - iko chini yammHg 60), na kizunguzungu au kuchanganyiwa; anaweza hata kupoteza fahamu. Ni lazima uchukue hatua mara moja ili kuokoa maisha yake.

20.3.2 Ujumbe muhimu kwa wanawake baada ya mimba kutoka pekee yake au uliopangwa

20.3.4 Matibabu ya rufaa ya awali katika dharura