20.3.4 Matibabu ya rufaa ya awali katika dharura

Matibabu ya dharura ya wagonjwa walio katika mshtuko ni pamoja na kuanzisha utiliaji dawa mishipani, yaani kupeleka kiowevu kilichofishwa vijidudu kinachoitwa Salini ya kawaida au kiowevu cha unyonyeshaji cha Ringer, moja kwa moja ndani ya mshipa ili kuchukua nafasi ya viowevu vya damu na chumvi ambavyo vinapotezwa kupitia uvujaji wa damu nzito. Utajifunza nadharia ya jinsi ya kufanya hivi katika Kipindi cha 22 cha Moduli hii, na katika mafunzo yako ya utendaji. Mara tu utiliaji wa dawa mishipani unapokuwa tayari, lazima upeane rufaa ya dharura ya wanawake kwenye kituo cha afya kilicho karibu

Mchoro 20.3 Mlalishe hivi mwanamke anayevuja damu na umsaidie haraka kupata utunzaji wa dharura.

Wakati wa kumsafirisha, hakikisha kuwa umemlalisha anavyofaa na kichwa chake kikiwa mahali palipo tambarare ( usitumie mto) na miguu yake ikiwa imeinuliwa na kuegemezwa (tazama Mchoro 20.3). Hali hii husaidia shinikizo lake la damu kutoshuka zaidi. Ikiwezekana, unapaswa kuandamana naye hadi kituo cha afya ili kuendeleza utiliaji wa damu kwenye mishipa na mfuko wa kiowevu cha IV kikishikiliwa juu yake. Ikiwa huwezi kwenda naye, eleza atakayeandamana naye umuhimu wa kumweka mama na mfuko katika mahali paliposhauriwa; Pia mjulishe jinsi ya kufunga tyubu wakati kiowevu kimeisha katika mfuko wake. Kwa kawaida, tuma mtu mwenye afya andamane naye anayeweza kutolea damu ikiwa atahitaji kuongezwa damu afikapo kituo cha afya.

Hakikisha kuwa umeandika barua ya rufaa

  • Je, unakumbuka maelezo haya? (ulijifunza haya katika Kipindi cha 13).

  • Barua ya rufaa inapaswa kuwa na jina, miaka na anwani ya mgonjwa; historia yoyote ya matibabu au ya kibinafsi ambayo inahusu hali yake ya kisasa; maelezo wazi ya dalili na ishara; maelezo ya matibabu yoyote umefanya; na sababu zako za kumpa rufaa kwenye kituo cha afya. Kumbuka kutia sahihi barua na kuandika tarehe kisha ueleze jinsi utakavyopatikana ili uweze kufuatilia mgonjwa baadaye.

    Mwisho wa jibu

20.3.3 Utunzaji wa kufuatilia baada ya kutoa mimba

20.4 Visababishi vingine vya kuvuja damu mapema wakati wa mimba