20.4.1 Mimba iliyotungika nje ya uterasi

Iwapo utashuku mimba isiyo kuwa katika sehemu yake lazima umtume mjamzito ili afanyiwe utathmini na kutibiwa kwenye kituo cha afya kilichoko karibu.

Mimba iliyotungwa nje ya uterasi ni wakati mimba huwa nje ya nafasi katika emdometria ya uterasi. Eneo la kawaida zaidi ya mimba isiyo kuwa katika sehemu yake ni neli ya falopio (jozi za neli zinazoshikanisha uterasi na undani wa fumbatio, kila moja kuishia karibu na ovari kwa upande huo. Tazama nyuma kwa Michoro ya 3.3 na 5.3 kwenye Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu ya 1, ili kujikumbusha anatomi ya uterasi na viungo vilivyokaribu. Uwezekano wa sehemu zingine ni tishu unganishi za ovari, ovari, na nafasi katika fumbatio iliyozunguka uterasi.

Ikiwa embrio itajikolea katika neva ya falopio, haitaweza kushikilia fetasi inayoendelea kuwa zaidi ya wiki chache za kwanza. Kuna uwezekano wa hatari kwamba neva itapasuka na mwanamke ataanza kuvuja damu ndani ya fumbatio. Hii ni hali ya kuhatarisha maisha inayosababisha mshtuko, ambayo ni lazima itibiwe kwa haraka ili kukomesha uvujaji wa damu. Dalili za kawaida za mimba isiyokuwa katika sehemu yake ni maumivu ya sehemu ya chini ya fumbatio, hedhi iliyochelewa, na kuvuja damu ukeni au kwa undani.

20.4 Visababishi vingine vya kuvuja damu mapema wakati wa mimba

20.4.2 Mimba isiyokuwa ya kawaida