20.4.2 Mimba isiyokuwa ya kawaida

Kila utakapo shuku mimba isiyokuwa ya kawaida, lazima umpeleke mama kwenye kituo cha afya haraka iwezekanavyo.

Sababu nyingine ya kuvuja damu mapema wakati wa ujauzito ni mimba isiyokuwa ya kawaida, ambayo ulijifunza katika Kipindi cha 10. Unaweza kupatana na tatizo hili mara kwa mara. Ina dalili ya ukuaji usiokuwa wa kawaida wa tyuma ulioundwa kutokana na plasenta ya baadaye mapema wakati wa awamu ya kwanza ya mimba. Uterasi hujazwa na tishu iliyoonekana kama zabibu na kuwa kubwa kuliko ukubwa utakaofikia kwa hatua kamili ya mimba ya kawaida (Mchoro 20.4).

Mchoro 20.4 Mimba isiyokuwa ya kawaida (tyuma) ina kuwa kwa uterasi badala ya mtoto.
  • Je, unaweza kukumbuka dalili za mimba isiyokuwa ya kawaida?

  • Mpigo wa moyo wa fetasi hayawezi kusikika. Huwezi kuhisi mtoto unapogusa fumbatio la mama. Mwanamke amehisi kichefuchefu wakati wote wa ujauzito. Ana doa la damu na tishu inayofanana na kicha cha zabibu unaotoka ukeni.

    Mwisho wa jibu

Mojawapo ya matatizo yanayoogopesha katika mimba isiyokuwa ya kawaida ni kunaweza kusababisha utokaji wa damu nyingi na kuweza kusabisha kifo cha mama. Ikiwa mama atakuwa anatokwa na damu ukeni, anza kwa kutia viowevu ndani ya mshipa (kama ilivyoelezwa katika Kipindi cha 22 na mazoezi katika vitendo vyako vya ujuzi) kabla ya kumpa rufaa. Kiowevu kinapaswa kutiririka matone 60 kwa dakika. Mama anapaswa kupelekwa katika kituo cha afya na watu wazima wenye afya ambao wanaweza kumtolea damu.

20.4.1 Mimba iliyotungika nje ya uterasi

20.5 Upangaji uzazi baada kutoa mimba