20.5 Upangaji uzazi baada kutoa mimba

Katika sehemu ya mwisho ya kipindi hiki, tunaingia kwa haja ya kupanga uzazi baada ya kutoa mimba. Katika matukio mengi, utoaji wa huduma ya dharura baada ya kutoa mimba unaweza kuwa mojawapo ya matukio ambayo mama na mpenzi wake uwasiliana nayo na mfumo wa huduma ya afya. Hivyo basi, inawakilisha fursa muhimu kwa kutoa taarifa na huduma ya upangaji uzazi.

Upangaji uzazi baada ya kutoa mimba inapaswa kuwa ni pamoja na vijenzi vifuatavyo:

  • Kushauri kuhusu mahitaji ya kupanga uzazi kulingana na malengo ya uzazi wa mteja
  • Maelezo na ushauri kuhusu njia zote zilizopo, sifa zao, zenye kuleta matokeo yanayotarajiwa, na madhara (tazama mchoro 20.5)
  • Uchaguzi kati ya utaratibu (kwa mfano, wa muda mfupi na wa muda mrefu, yenye homoni, na isiyo na homoni)
  • Kuhakikisha kwamba unaendelea kutoa upangaji uzazi, ili mama asiishiwe na ulinzi:
    • Kupatikana kwa huduma ya kufuatilia
    • Taarifa kuhusu mahitaji ya kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.
Mchoro 20.5 Baadhi ya mbinu za kuzuia mimba.

Upangaji uzazi baada ya kutoa mimba pia inapaswa kuzingatia utathmini wa mtu binafsi kwa kila hali ya mwanamke: tabia yake binafsi, hali ya kliniki, na uwezo wa utoaji huduma katika jamii ambako anaishi. Utajifunza kuhusu haya yote kwa undani katika Moduli ya Upangaji Uzazi katika mtaala huu. Wanawake wengi watapata upangaji uzazi baada ya kutoa mimba wakiwa katika kituo cha afya cha ngazi ya juu, lakini wachache wanaweza kuwa wametoka mapema. Unaweza pia kuhitajika kuendelea kuwapa mbinu za kuzuia mimba wakiwa katika jamii yako. Hivyo hii ni eneo moja unajukumu kubwa kwa utoaji wa huduma kwa wanawake waliotoa mimba.

20.4.2 Mimba isiyokuwa ya kawaida

20.5.1 Wakati wa kuanza upangaji uzazi