Maswali ya kujitathmini ya kipindi cha 20

Kwa kuwa sasa umekamilisha kipindi hiki, unaweza kutathmini jinsi ulivyotimiza malengo yake ya somo kwa kujibu maswali yafuatayo. Andika majibu yako kwenye Shajara yako ya Somo na uyajadili na Mkufunzi katika Kipindi Saidizi kijacho. Unaweza kulinganisha majibu yako na nakala kwenye Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.

Swali la Kujitathmini 20.1 (linatathmini Malengo ya Somo 20.1, 20.3 na 20.5)

Kati ya kauli zifuatazo ni zipi si sahihi? Katika kila kauli, eleza ni nini sio sahihi.

  • A.Hakuna haja ya kupeana rufaa kwa hali zote za utoaji mimba usiokamilika kwenye kituo cha afya cha ngazi ya juu.
  • B.Katika utoaji wa mimba uliokamilika tishu iliyo ndani ya uterasi imetolewa na seviksi imefungika.
  • C.Wanawake ambao utoaji wao wa mimba umekamilika hawatapata mimba tena kwa miezi michache.
  • D.Baada ya kutoa mimba, mwanamke anapaswa kushauriwa acheleweshe ujauzito unaofuata hadi apone vizuri.

Answer

A si sahihi. Wanawake wote walio na utoaji wa mimba usiokamilika wanapaswa kupewa rufaa kwenye kituo cha afya cha ngazi ya juu. Ukiacha bila matibabu kwa muda, kunao ongezeko la hatari wa kuathiriwa na maambukizi na hii inaweza kuhatarisha maisha ya mwanamke.

B ni sahihi. Katika utoaji wa mimba uliokamilika tishu iliyo ndani ya uterasi imetolewa na seviksi imefungika.

C si sahihi. Wanawake ambao utoaji wao wa mimba umekamilika wanaweza kupata mimba haraka, kwa sababu uwezo wa kuzaa hurudi kwa muda wa kati ya wiki mbili na mpaka wiki nne.

D ni sahihi. Baada ya kutoa mimba, mwanamke anapaswa kushauriwa acheleweshe ujauzito unaofuata hadi apone vizuri.

Mwisho wa jibu

Kwanza Soma Kisa cha Somo la 20.1 kisha ujibu maswali yanayofuata.

Uchunguzi Maalum 20.1. Bi. X

Bi X ana umri wa miaka 26 na ameolewa kwa muda wa miaka 4. Yeye ana mtoto mmoja aliyezaliwa miaka 3 iliyopita na anatumai kuwa ni mjazito tena. Bi X anasema kuwa anao uchungu katika sehemu ya chini ya fumbatio lake na alianza kuvuja damu siku mbili zilizopita. Unapomchunguza anao mpigo wa kasi kwa mshipa wa mipigo 100 kwa dakika na shinikizo la damu la mmHg 110/60. Pia anayo konjaktiva yenye rangi ya buluu hafifu na uchungu mdogo wa sehemu ya chini ya fumbatio linapoguswa.

Swali la Kujitathmini 20.2 (linatathmini Malengo ya Somo 20.2 na 20.4)

  1. Je, visababishi vya uvujaji damu katika awamu hii ya mapema katika uajuzito wake ni nini?
  2. Je, dalili zingine zake zinaweza kuashiria ni nini kinachotendeka?
  3. Toa sababu zako ilikubaini ikiwa itakuwa salama kumpa rufaa kwenye kituo cha afya cha ngazi ya juu.
  4. Ikiwa utampa rufaa, je, utafanya nini kabla ya kupelekwa?

Answer

  1. Visababishi vinavyoweza kusababisha uvujaji damu kwa wanawake kama Bi X katika awamu ya mapema ya ujauzito ni:
    • Kutoka kwa mimba pekee yake (uharibikaji wa mimba)
    • Mimba iliyotungwa nje ya uterasi
    • Mimba isiyokuwa ya kawaida.
  2. Kwa kuwa anayo maumivu katika sehemu ya chini ya fumbatio, mpigo wa kasi wa mshipa, shinikizo la damu la chini (mmHg110/60), na konjaktiva ya rangi ya buluu hafifu (ishara ya anaemia) huashiria kuwa anaelekea kuwa na mshtuko kwa sababu ya kupoteza damu.
  3. Anapaswa kupewa rufaa kwenye kituo cha afya cha ngazi ya juu kwa sababu anaweza kupoteza fahamu na kufa; tayari amekuwa akivuja damu kwa muda wa siku mbili.
  4. Kabla ya kumtuma kwenye kituo cha afya, unapaswa:
    • Kunza utiliaji wa dawa mishipani ili kuchukua nafasi ya viowevu vilivyopotezwa kupitia uvujaji damu.
    • Mweke kwenye gari na kichwa chake kikiwa mahali palipo tambarare
    • Apelekwe na mtu ambaye anweza kumtolea damu ikiwa atahitaji kuongezwa damu.
    • Andika barua ya rufaa inayoeleza mambo yote muhimu

Mwisho wa jibu

Swali la kujitathmini 20.3 (linatathmini Malengo ya Somo 20.5)

Taja mambo matatu mazuri ambayo upangaji uzazi baada ya kutoa mimba itajumuisha.

Answer

Ulipaswa tu kutambua mambo matatu kati ya zifuatazo, lakini huduma nzuri ya upangaji uzazi baada ya kutoa mimba itajumuisha:

  • Kushauri kuhusu mahitaji ya mbinu za kuzuia mimba kwa matakwa ya malengo ya mteja
  • Taarifa na ushauri kuhusu njia zote zinazopatikana, sifa zake, matokeo yanayofaa, na madhara
  • Uchaguzi miongoni mwa mbinu (kwa mfano, wa muda mfupi na wa muda mrefu, wa homoni na usio wa homoni)
  • Udhibitisho wa kuleta kontraseptivu, ili mwanamke asikose ukingaji
  • Habari kuhusu mahitaji ya kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 20