22.1.3 Mbinu safi za matibabu ya kudungia viowevu mishipani.
Unapojitayarisha kumpa mtu matibabu ya kudunga viowevu mishipani yake, ni sharti kila kitu kiwe safi na utumie mbinu safi (zisizo na uchafuzi wa kiini cha maradhi) mara nyingi iwezekanavyo. Jambo hili linaweza kuwa gumu kufanya katika maeneo ya mashambani lakini ukifuatilia maelekezo yaliyo kwenye Kisanduku 22.1, unaweza kupunguza hatari ya maambukizi.
Kisanduku 22.1 Kuzuia maambukizi wakati wa matibabu ya kudungia viowevu mishipani
- Hatua muhimu zaidi ni kunawa mikono kabisa kwa sabuni na maji safi kwa angalau dakika mbili kabla na baada ya kushika mgonjwa au kifaa chochote kisafi.
- Tumia alkoholi kupanguza sinia au sahani utakayowekea vifaa vyako au (ikiwa haipatikani) safisha sinia kwa sabuni na maji na uhakikishe kuwa imekauka vya kutosha kabla ya kuitumia.
- Vaa glavu safi au zilizosafiswa kabisa. Kwa kuwa utagusa damu ya mgonjwa huyu, ni lazima uvae glavu kila wakati.
- Kanula, neli ya sindano ya mshipa na glavu za upasuaji huwa zimefungwa kwa plastiki safi au kifurushi cha karatasi. Pande za ndani za vifurushi hivi huwa safi hivyo zinaweza kufunguliwa na kutandazwa ili kutumika kama sehemu safi ya kuweka vifaa hadi utapovihitaji tena.
- Mgonjwa anapaswa kuwa amelazwa kwa hali ya kutulia. Panguza ngozi yake kwa alkoholi au sabuni na maji kwenye sehemu ambayo kanula itaingizwa mishipani.
- Fungua kifurushi safi kilichofunika neli ya kutilia viowevu kisha uiunganishe na kifuko cha viowevu. Tundika kifuko hiki kwenye kiopoo kilicho ukutani juu ya mgonjwa au uulize mtu yeyote akishikilie juu ya mgonjwa. Hakikisha kuwa sehemu ya mwisho ya neli itakayoshikanishwa na kanula imewekwa safi bila kuguswa.
22.1.2 Kutayarisha vifaa vya matibabu ya kudungia viowevu mshipani